Nairobi – Nchini Kenya wakati serikali ikiendelea kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa macho mekundu ambao umeambukiza watu zaidi ya elfu moja, imetangaza kurejesha namba ya dharura iliyokuwa inatumika wakati wa janga la Uviko 19, kama mkakati wa kukabiliana na dharura na kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.